Majina ya nasaba
Nasaba
Nasaba ni uhusiano wa kizazi baina ya watu. Uhusiano huu unaweza kuwa katika familia au ukoo mmoja au uzao mmoja.
1. Mama/nina: Mzazi wa kike.
2. Baba: Mzazi wa kiume.
3. Kaka: Ndugu wa kiume.
4. Dada: Ndugu wa kike.
5. Nyanya/Bibi: Mama/Mzazi wa kike wa baba au mama.
6. Babu: Baba/Mzazi wa kiume wa mama au baba.
7. Mjukuu: Mtoto wa mwana.
8. Kitukuu: Mwana wa mjukuu.
9. Kilembwe: Mwana wa kitukuu.
10. Kilembwekeza/kining’ina: Mwana wa kilembwe.
11. Kitojo : mtoto wa kilembwekeza.
12. Ami/amu: Kaka wa baba.
13. Shangazi: Dada wa baba.
14. Mjomba/hau: Kaka wa mama.
15. Halati/hale: Dada wa mama.
16. Mkazahau/Mkazamjomba: Mke wa mjomba.
17. Mkazamwana: Mke wa mwana.
18. Mavyaa: Mama wa mume.
19. Bavyaa: Baba wa mume.
20. Mamamkwe: Mama wa mke.
21. Babamkwe: Baba wa mke.
22. Mcheja: Baba au mama wa mke au mume (mkwe).
23. Kivyere : Jina linalotumika kuitana wazazi wa mke na wazazi wa mume
24. Mpwa: Mtoto wa dada wa mtu mwanamume, jina analotumia mjomba kumwita mtoto wa dada yake.
25. Mkoi: Mtoto wa shangazi au mjomba
26. Binamu: Mwana wa kiume wa ami (ami/amu ni Ndugu wa kiume wa baba.)
27. Bintiamu: Mwana wa kike wa ami.
28. Shemeji: Ndugu wa mke au ndugu wa mume. Pia ni Rafiki wa kiume wa mume au rafiki wa kike wa mke.
29. Mama wa kambo: Mama asiyekuzaa lakini anakulea.
30. Baba wa kambo: Baba asiyekuzaa
31. Umbu: Jina waitanalo kaka na dada.
32. Ndugu mlungizi: Ndugu anayekufuata nyuma. (mdogo wako anayekufuata)
33. Wifi:
(a) Mke wa kaka. Iwapo wewe ni msichana, mke wa kaka yako utamwita wifi.
(b) Dada wa mume: Iwapo msichana ameolewa dada wa mumewe atamwita wifi.
34. Mwamu/mlamu:
a) Kaka wa mke. Mwanamume akioa, kaka wa mkewe atamwita mlamu.
b) Mume wa dada: mvulana au mwanamume atamwita mume wa dadaye – mlamu.
35. Mwanyumba: Wanaume waliooa katika familia moja.
36. Mkemwenza/mitara: Jina wanalotumia wanawake walioolewa na mwanamume mmoja.
37. Kifungamimba/ kitindamimba/ mzuwanda: Mtoto wa mwisho kuzali- wa katika familia.
38.Mwanambee/kifunguamimba/kichinjamimba: Mtoto wa kwanza kuzaliwa katika familia.
39. Nyanyamkuu: Mama wa nyanya.
40. Babu mkuu: Baba wa babu.
41. Maharimu: Mtu usiyeweza kumwoa au kuolewa naye kwa sababu ya uhusiano wa nasaba.
42. Mnuna: Ndugu ndugu mdogo.
s.kitaly86@gmail.com
Mama mdogo ni nani
JibuFutanaomba kujua babu wa baba yangu nitamuita nani?
JibuFuta