UHIFADHI WA FASIHI SIMULIZI
Ili kitu kidumu ni lazima kihifadhiwe; fasihi simulizi kama
sanaa kutokana na umuhimu wake katika jamii nayo huhufadhiwa kwa ajili ya faida
ya kizazi kijacho. Katika mada hii utaweza kujifunza umuhimu wa fasihi simulizi
katika jamii. Utajifunza njia mbalimbali zitumikazo katika uhifadhi wa fasihi
simulizi pia utaweza kubainisha ubora na udhaifu wa kila njia.
Umuhimu
wa kazi za fasihi simulizi
Ingawa
kila utanzu wa fasihi una umuhimu wake, kwa pamoja tanzu zake zote zina umuhimu
mkubwa katika jamii.
v Fasihi hutumika kama chombo cha kuwaelimisha
watu. Kupitia
fasihi andishi na fasihi simulizi, watu hupata maarifa ya kutambua mambo maovu
na namna ya kuyakwepa. Licha ya haya, wanajamii hujifunza njia za kujitawala,
kuzalisha mali na kuishi kwa misingi ya haki, usawa na demokrasia.
v Fasihi ni nyenzo ya kutoa mafunzo kuhusu mambo
kama vile historia, dini, siasa, jiografia na tiba. Kwa hiyo watu hujifahamisha juu ya maumbile
na asili yake, mazingira, utawala, uchumi, sheria n.k. kwa kutumia fasihi
simulizi au fasihi andishi.
v Fasihi huwapa watu mazoezi na kuimarisha uwezo
wao wa kuzungumza kwa ufasaha, kuimba nyimbo kwa ufundi, kuigiza mambo kwa ustadi, kucheza
ngoma kwa umahiri, kughani mashairi kwa mvuto na kusimulia matukio kwa mtindo
ufaao.
v Fasihi hufahamisha, huhifadhi na hurithisha
mambo kuhusu utamaduni kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Mambo hayo ni pamoja na mila, desturi,
falsafa, imani na itikadi. Pia hudumisha maarifa ya kijadi kama vile tiba,
sayansi ya kilimo, uhifadhi wa mazingira na sayansi ya utabiri wa hali ya hewa.
v Hutumika kama chombo cha kuburudisha na
kupumbaza.
Watu wanaposoma kazi mbalimbali za fasihi hupata, msisimko wa kimwili na
kiakili. Kadhalika fasihi hugusa hisia za watu na kuwafanya wafurahi au
wahuzunike.
v Fasihi hudumisha na kukuza lugha. Watu hupanua msamiati wao na miundo ya lugha
kupitia kazi zake. Hivyo fasihi inakuwa kama hazina ya maneno na dafina ya
kanuni za kisarufi.
Kutokana
na umuhimu huu ndio maana fasihi huhifadhiwa ili isipotee. Na uhifadhi huu
hufanyika kwa njia mabalimbali.
1.
Kichwani
Hii ndio njia ambayo imekuwa ikitumiwa
kuhifadhi kazi za fasihi tangu kale na inaendelea kutumika hadi leo. Kwa
kutumia njia hii kazi ya msanii hukaa kwenye ubongo wa msanii, naye huweza
kuiwasilisha kazi hiyo, wakati wowote bila gharama yoyote.
Ubora
wake
v Huweza kuwasilishwa muda wowote.
uwasilishaji wa kazi hiyo unaweza kufanyika wakati wowote bila kuhitaji
kufanyika maandalizi yoyote, hususani ya kiufundi.
v Hakuna gharama yoyote wakati wa uwasilishaji
wa kazi ya fashi. Msanii hahitaji kugharimia kitu chochote ili waweze kuitoa
kichwani, ni uamzi wake tu, anaweza kuimba papo kwa papo.
v Kazi ya fasihi iliyohifadhiwa kichwani ni hai.
Hii ni kwa sababu msanii anakuwa ana kwa ana na hadhira yake. Kutokana na
matumizi ya mbinu tofauti za kisanaa kama vile kucheza, kubadili sauti,
miondoko na mengineyo mengi, kazi yake inapata uhalisia zaidi mbele ya hadhira.
Udhaifu wake
v Simulizi huweza kupotea kwa urahisi,
kwa mtu aliyehifadhi kumbukumbu za akili zinaweza kupungua,au kufifia au fanani
kufariki dunia. Hali hii ikitokea simulizi aliyoihifadhi katika ubongo/kichwa
chake nayo hupotea.
v Huwa ni rahisi kubadili mambo muhimu katika
simulizi hiyo. Hii inatokea pale ambapo msanii anasahau baadhi ya maneno
kutokana na umri wake au sababu nyinginezo.
v Kuna tatizo lakupata watu wanaoweza kuhifadhi
kazi hizo
kutokana na mazingira na mabadiliko yanayotokea katika jamii/ maisha.
2.
Njia ya maandishi
Kutokana na maendeleo
ya sayansi na teknolojia, fasihi simulizi inahifadhiwa katika maandishi
kwaajili ya kumbukumbu za baadae. Njia hii imeanza kutumika baada ya watu kujua
kusoma na kuandika. Uhifadhi wa kazi za fasihi kwa njia hii hupitia njia mbili
kubwa.
* Hatua ya kwanza ni kubuni kisa au wazo.
* Hatua ya pili ni kuliweka wazo hilo katika
maandishi.
Kazi za fasihi simulizi zinazoweza kuhifadhiwa
katika maandishi ni hadithi, nyimbo, mashairi, ngonjera, majigambo n.k
Ubora wake
v Hudumu kwa muda mrefu, Kazi iliyohifadhiwa katika maandishi inaweza
kudumu kwa muda mrefu
v Huwafikia watu wengi zaidi, Kazi iliyohifadhiwa inaweza kufikia hadhira
hata ya mbali na aliko msanii/ fanani.
v Fasihi simulizi ikihifadhiwa katika maandishi
haipotezi fani na maudhui yake, Kazi iliyohifadhiwa katika maandshi haipotezi fani yake na
maudhui yake bali huendelea kuwa katika asili yake ya awali hadi msanii
atakapoamua kuibadilisha.
Udhaifu wake
v Njia hii hutumiwa na watu wachache hususani
wale wanaojua kusoma na kuandika. Fanani na hadhira wanaoweza kutumia njia hii ni wale tu
wanaojua kusoma na kuandika
v Ni gharama kubwa kuhifadhi fasihi simulizi
katika maandishi.
Msanii atalazimika kununua vifaa vinavyohitajika katika maandishi ambavyo ni
kalamu, karatasi, meza, gharama za uchapaji n.k.
v Fasihi simulizi ikihifadhiwa katika maandishi
hukosa uhai wake, Uwasilishaji wake si hai kwani hakuna kuonana ana kwa ana kati
ya hadhira na fanani. Kwa hiyo msomaji hawezi pata vionjo vya msanii hivyo
itambidi ajibunie yeye mwenyewe.
v Huwa ni mali ya msanii, fasihi simulizi ni mali ya jamii lakini
ikishahifadhiwa katika maandishi inakuwa ni mali ya yule aliyeihifadhi kazi
hiyo katika maandishi badala ya jamii nzima.
v Si kila kitu kinaweza kuhifadhiwa katika
maandishi,
maandishi kuna mambo ambayo kamwe hayawezi kuhifadhiwa katika maandishi. Mambo
hayo ni yale yanayohusiana na utendaji ikiwemo sauti, vitendo, toni, kiimbo
n.k.
v Haiwezi kubadilika kulingana na wakati na
mazingira, hivyo hudumu katika hali yake ileile hata kama kuna makosa
yaliyotendeka na msanii hayawezi kurekebishwa mpaka toleo jingine.
3.
Njia ya vinasasauti
Vinasasauti ni
miongoni mwa vyombo vinavyotumika kuhifadhi kazi za fasihi simulizi. Hii ni
njia iliyoendelea kuliko ile ya maandishi, vinasa sauti hushika sauti na vidoko
vyake. Hivyo ili hadhira ipate kazi ya fasihi simulizi lazima anunue kanda
hizo.
Ubora wake
v Kazi ya msanii huweza kuwafikia watu hata
walio mbali na alipo mtunzi.
v Ikihifadhiwa katika vinasasauti kama vile
tepurekoda au CD ubora wake huwa haupotei wala kuharibika endapo vifaa hivyo
vitatunzwa vizuri.
v Sauti ya mtunzi unaiskia moja kwa moja
v Unaweza kusikia vionjo vya msanii
Udhaifu wake
v Kanda za kunasia sauti hushika sauti tu, hapa sauti huweza kusikika lakini matendo
hayawezi kushikwa, kwa namna hiyo huweza kuathiri uhifadhi na utoaji wa kazi ya
fasihi simulizi.
v Kukosekana kwa ushiriki wa hadhira, hapa
sauti ya fanani husikika lakini haiwezekani kuonana ana kwa ana kati ya fanani
na hadhira. Hivyo hadhira hushiriki kwa
kusikiliza sauti tu.
v Ni gharama kubwa kuhifadhi kazi ya fasihi
simulizi kwa njia hii, kwanza huwa ni gharama kununulia kinasasauti pamoja na kununua
kanda zenyewe, betri, n.k.
v Uwasilishaji wake si hai, ingawa unaweza sikia sauti ya msanii au
wahusika lakini hawawezi kuonekana na hata hivyo haiwezi kubadilika kulingana
na wakati na mazingira.
v Huwa ni mali ya msanii, Kazi yoyote ya kifasihi simulizi
inapohifadhiwa katika vinasasauti, kwa mfano nyimbo, huwa ni mali ya msanii
husika, mtu yeyote haruhusiwi kuitumia kama mali yake binafsi bila kuruhusiwa
na msanii.
4.
Njia ya tarakilishi
Njia hii imeanza kutumika katika miaka ya hivi karibuni baada ya
watu kuanza kujua na mna ya kutumia kompyuta.
Ubora wake
v Njia hii ni ya uhakika zaidi kwa vile shuguli
za kisanaa zinazohusika huhifadhiwa katika kompyuta na hutolewa pale zinapokuwa
zinahitajika.
Udhaifu
v Msanii au wasanii wanohusika hawawasiliani na
hadhira papo kwa papo. Hivyo hadhira hukosa kuuliza maswali katika vipengele
vinavyotatiza.
v Hutumiwa na watu wachache, Ili kuhifadhi kazi ya fasihi kwa kutumia
njia hii ni sharti msanii awe anajua kutumia kompyuta vilevile hadhira lazima
ajue kutumia kompyuta.
v Njia hii ina gharama kubwa, ili uweze kuhifadhi fasihi simulizi kwa njia
hii ni lazima uwe na kompyuta na ukizingatia kwamba kununua komputa ni gharama
kubwa. Hivyo huwanufaisha tu wale wenye vyombo hivi vya kisasa.
v Njia hii inatumika zaidi mjini, ili kutumia kompyuta lazima mtumiaji awe na
ujuzi na pia kuwepo na umeme hivyo wale wa vijijini na maeneo ambayo hakuna
umeme hawawezi kupata kazi ya fasihi simulizi iliyohifadhiwa kwa njia hii.
5.
Njia ya kanda za video,
televisheni na filamu za sinema.
Msanii huweza kutumia kanda ya video kuhifadhi kazi yake. Njia
hii huweza kurekodi sura na sauti ya fanani. Hivyo kwa kutumia njia za filamu,
za sinema na video tunawezakuhifadhi na kuonesha kazi za fasihi simulizi.
Ubora wake
v Kwanza wasanii na vifaa wanavyotumia
huonekana,
v Sauti zao na milio ya ala wanazotumia husikika
na pia huonekana kwa hadhira. Hii angalau huipa uhai kazi ya msanii mbele ya
hadhira.
v Huweza kudumu kwa muda mrefu endapo kanda ya
video iliyotumika kuhifadhi kazi ya msanii itatunzwa vizuri.
Udhaifu wake
v Uhifadhi wa njia hii unagharama sana, msanii atahitajika kununua, kanda ya video,
kumlipa mpiga picha na mzalishaji pia.
v Watu wanoweza kunufaika na njia hii ni
wacheche mno
na wengi wao ni wale wenye uwezo wa kumiliki televisheni ambao kimsingi
hupatikana maeneo ya mijini.
v Ingawaje hadhira wanaweza kumwona msanii
lakini hawawezi kuwasiliana nae ana kwa ana, hivyo kukosa kuuliza swali pindi
wanapohitaji kufanya hivyo.
Umuhimu wa kuhifadhi kazi za Fasihi Simulizi
v Ni muhimu
kuzihifadhi kazi hizo zisiharibike wala kupotea ili ziendelee kutumika kutoka
kizazi kimoja hadi kingine.
v Ni muhimu
kuzihifadhi ili ziendelee kuwepo ili kuhifadhi utamaduni wetu na huku
vikitumika kama vivutio kwa jamii na wageni/watalii.
v Kazi za fasihi
simulizi kwa upande mwingine ni sehemu ya ajira. Kwa mfano, shughuli
mabalimbali za kisanaa kama vile ngoma, maigizo na utunzi wa vitabu,
vinawapatia vipato baadhi ya wasanii. Hivyo ni muhimu zihifadhiwe.
v Kazi za fasihi
simulizi pia ni kichocheo cha umoja na maelewano miongoni mwa jamii.
Yote hayo kwa ujumla wake yanabainisha
kuwepo na haja ya
kuendelea kuzikusanya, kuzifanyia kazi, kuziendeleza, na
kuzihifadhi
kazi za fasihi simulizi.
Asante sana.je,naweza kupata masomo mengine ya mr.mshiu?
JibuFuta